Maandamano yanayoendelea nchini yana madhara kuliko faida.

By KUZANEWSTV.CO.KE
24th July, 2023

Ipo haja ya serikali ya Kenya kwanza na ile serikali pinzani ya Azimio la umoja kuja pamoja na ksitisha maandamano nchini.Ghasia za maandamano zinazoshuhudiwa nchini humkandamiza yule mwananchi wa chini.Vifo ,ajali,uharibifu wa mali za ummah sio suluhu bali suluhisho ni pande zote mbili kuja pamoja na kupata njia mwafaka ya kufufua uchumi wa Kenya .

Wakenya wengi wapinga kauli ya senator wa Nairobi Bw Edwin sifuna kwa kutangaza maandamano ya siku tatu mutawalia . Ukweli wa maandamano haya hayatobadilisha gharama ya maisha na kurudi chini bali itasalia pale pale na kumkandamiza mwananchi wa Kenya.Hivyo basi kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga ni asitishe maandamano hayo na akabiliane na serikali ya Rais Ruto kwa mazungumzo ya dayolojia kwanza kabla ya kuamuru maandamano ya amani yanayogeuka kuwa fujo na ghasia.

Polisi nao watumie silaha zao kwa njia inayosutahiki kwa maana hiyo hao ndio huchangia pakubwa katika kuleta ghasia katika maandamano ya amani kama yanavyodaiwa na Serikali pinzani ya Azimio la umoja.Wakenya wakiwa barabarani wakiaandamana polisi huwarushia vitoza machozi na hatimaye fujo na ghasia za uharibifu wa mali na vifo vikishuhudiwa .

Twaomba maandamano hayo yalitangazwa rasmi kuwa ni awamu ya tatu ni kusitishwa maana wakenya wanashuhudia hali ngumu ya maisha inayowaathiri wengi na kupelekea idadi ya wakenya wanaokosa mlo kwa siku kuongezeka kutokana na bei ya vyakula kupandishwa Kila uchao.


Mohammed Ismail
Mwanahabari & mwanafunzi
Runinga ya Kuza

Tags:

GAZETI LA NURU GAZETI LA NURU

This site was designed with Websites.co.in - Website Builder

WhatsApp Google Map

Safety and Abuse Reporting

Thanks for being awesome!

We appreciate you contacting us. Our support will get back in touch with you soon!

Have a great day!

Are you sure you want to report abuse against this website?

Please note that your query will be processed only if we find it relevant. Rest all requests will be ignored. If you need help with the website, please login to your dashboard and connect to support